Isaiah 8:7-9


7 akwa hiyo Bwana yu karibu kuleta dhidi yao
mafuriko makubwa ya Mto:
Yaani Frati.

yaani mfalme wa Ashuru na fahari yake yote.
Yatafurika juu ya mifereji yake yote,
yatamwagikia juu ya kingo zake zote,

8 cna kufika hadi Yuda, yakizunguka kwa kasi juu yake,
yakipita katikati na yakifika hadi shingoni.
Mabawa yake yaliyokunjuliwa
yatafunika upana wa nchi yako,
Ee Imanueli!”
Imanueli maana yake Mungu yu pamoja nasi.


9 eInueni kilio cha vita, enyi mataifa,
na mkavunjwevunjwe!
Sikilizeni, enyi nyote nchi za mbali.
Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe!
Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe!
Copyright information for SwhKC